Home Lifestyle Wasifu Wake Aurlus Mabele (Aurlus Mabele Biography)

Wasifu Wake Aurlus Mabele (Aurlus Mabele Biography)

2169

Wasifu Wake Aurlus Mabele Almaarufu Mfalme Wa Soukous aliyeenda ulaya, kuishi Maisha bora na katambulisha mziki wa soukous kimataifa lakini Mungu si Athumani. Akamuchukulia huko. Yaani Mungu si kama mwanadamu hufanya mambo yake kwa wakati wake na kulingana na mapenzi yake.

Kwa mashabiki wa nyimbo za Lingala huwezi kukosa kusikia kwenye vinywa vyao wakilitaja jina la Aurlus Mabele almaarafu mfalme wa soukous .

Aurlus Mabele ambaye jina lake halisi ni Aurelien Miatsonamana alizaliwa Octoba ishirini, mwaka wa elfu moja miaka kenda hamsini na tatu katika wilaya Poto –poto nchini Kongo Brazaville. Kabla ya kuhamia katika mji mkuu wa Ufaranza, Parii, mwaka wa elfu moja mia kenda na themanini.

Yasemekana Mabele alipenda kusakata densi pamoja na kupiga gita kwa kazi ya juu akiwa na umri mdogo. Alijihusisha na makundi mbalimbali ya muziki nchini kwao na pia rafiki zake kutoka jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika enzi za kupigania Uhuru na pia vita baada ya Uhuru miaka ya tisini kati ya Lumumba ,Kasavubu, Moishe na wengine walipokuwa wakipigania kuongoza Kongo ya enzi zile.

Mwaka wa 1974, Mfalme wa soukous kama alivyojulikana na mashabiki wake kutokana na uimbaji na ucheshi wake akiwa jukwaani, alianzisha kundi la Ndimbola Lokela ambapo alipenda kucheza gita la besi na pia kubuni nyimbo mbalimbali. Wakati huo, alikuwa akiimba mara nyingi huko Martinique, Guadeloupe, Guyana na Reunion kwa usaidizi mkubwa wa Michel Nicole, ambaye aliandaa safari zake.

Mnamo mwaka 1987 Mabele pamoja na wenzake akiwemo –Diblo Dibala, Jean Baron na May Cacharel walianzisha kikundi cha Loketo inayomaanisha chezesha ‘hips zako’ hii ni baada ya kushiriki tamasha nyingi katika bara la ulaya mwaka wa 1986. Ili kuwa tofauti na kundi lao la kwanza akiwa na Diblo Dibala, wanaloketo wakatengeneza muziki maarufu wa soukous ambapo baadaye Mabele alitajwa kama mfamle. Hivyo basi ikapelekea msemo wa kuwa ‘’Aurlus Mabele ndiye mfalme wa soukous’’ jina ambalo aliitwa na mashabiki wake hadi kifo chake,japo wadukuzi wanasema haya hayakumfurahisha Diblo Dibla aliyejiona kama jogoo katika uga huu na kuwa Mabele ni mnuna wake kimziki ,hii ni kati ya sababu zilizosababisha mfarakano kati ya Diblo na Mabele miaka ya tisini.

Inasemekana Kuna wakati jamaa Hawa waliwasha moto katika club moja iitwayo kennel club maeneo ya San Francisco kwa unenguaji wa hips zao.

Jina hili la kilakabu la King of soukous alilipata kutokana na uimbaji na ucheshi wake akiwa jukwaani ambapo alipenda kujishaua na kujinadi kwa mapigo ya gita na miundoko ya kimaringo ya soukous kiwango cha kuwapiku si waasisi pekee bali pia wenzake wote katika kikundi.Mabele pia alipendwa na vidosho wengi akiwa jukwaani kutokana mtindo wke wa mavazi na tabasamu lake kila mara.

Kundi la Loketo lilipata nguvu na umaarafu zaidi wakati magwiji na wamanyi wa kucheza densi akiwemo Fred Mayunga,Lucien Bokilo,Mack Mackaire, sean Bilongo,Awilo Longomba na Komba Bello walipojiunga nalo jambo lililopelekea kundi hili kupata umaarafu si afrika ya kati na mashariki tu bali pia katikamaeneo mengi kule Ulaya na Marekani.

Nguli huyu wa miondoko ya soukous hatimaye alihamia Ufaransa na akaamua kuishi katika mji mkuu wa Parii kutokana na uzuri wake. Yasemekana pia sababu moja ya kuhamia Ufaranza hasa katika mji wa Parii ni yale ya maji kufuata mkondo kwani enzi hizo mababe wa nyimbo za lingala kama Papa Wemba aliyeanzisha Isifi Lokole tayari alikuwa amehamia huku miaka ya sabini. Sababu nyingine yasemekana ni shinikizo la kikundi kwani wenzake walihamia marekani uingereza.

Mnamo mwaka wa elfu moja mia tisa na tisini kulitokea kutoelewana kati yake na Diblo Dibla. Tokeo lake likawa kuvunjika kwa kukindi cha Lokote ijapokuwa baadaye walifanya kazi zingine na Dibala. Sababu kuu ya kukosana kwao yasemekana ni uchu wa kiwango cha juu alichokuwa nacho Mabele, aliwapenda wanenguaji wanadada hadi kujamiiana na wengine na kuwapa nafasi kubwa zaidi kundini jambo ambalo halikumfurahisha Dibala. Mchepuko ukaleta balaa babu!

Baada ya kusambaratika kwa kundi la lokote makundi mengine yalichibuka yakiwemo Soukous stars almaarufu Yondo Sisters, Lokasa ya mbongou na Ngouma Lokito. Katika uimbaji wake aliweza kuigiza katika majukwaa mengi Afrika na Uropa na kulingana na gazeti la Forbes Mabele aliweza kuuza zaidi ya album milioni kumi basi kumwingisha katika ulingo wa wanamuziki tajiri zaidi dunia japo ufasaka ulikuwa donda katila kuendelea kwake.
Wazungu wansema More Money, more problems. Daa! Katika miaka 25 ya kazi zake ameuza zaidi ya nakala milioni 10 za albamu dunia nzima na alisaidia kwa kiasi kikubwa katika kuitambulisha na kuisukuma vilivyo muziki wa soukous nje ya mipaka ya bara la Afrika .

Kwa kushirikiana na wapiga gitaa maarufu na wenye vipaji, ametengeneza dansi ya Kiafrika yenye ladha yake ya kipekee ya soukous kwa kutunga nyimbo kama vile Mousso Africa, Ivorian woman, Embargo, Betty De Asta, Evelyne, Loketo na kadhalika.

Mwanamuziki Mabele alianza kusumbuliwa na ugojwa wa Kiharusi na ugonjwa wa kupooza kwa miaka mitano, lakini aliweza kujipanga ili kufanya tamasha kadhaa na kundi zima la Loketo huko Ulaya kati ya mwezi Mei na Juni, 2009.

Kati ya nyimbo zilizomchoresha Mabele na wenzake katika kumbukumbu ya nyimbo za lingala ni pamoja na nyimbo kama vile Mousso Africa, Ivorian woman, Embargo, Betty De Asta, Evelyne, Loketo na kadhalika.
Baadhi ya albamu zake ni pamoja na Dossier X 2000, Compil two na Compil one za mwaka 1999. Zingine ni Tour de contrôle ya mwaka 1998, Best of Aurlus Mabele ya mwaka 1997, Génération-Wachiwa encaisse tout ya mwaka 1994, Stop Arretez ya mwaka 1992 na Embargo ya mwaka 1990.

Daa! Kifaransa balaa…lakini natumai mtanielewa…wenzetu kutoka ziwa Victoria wanasema, “Kiswahili si mdomo chetu,” hapa mambo si ya kitoto aisee. Yote ni hali ya malimwengu na lugha! Ingekuwa Kijerumani ningetamka kwa ufasaha sana. Kwa ufupi mimi nafahamu kijerumani sana! Sijigambi, ni ukweli. Wacha tuendelee basi!

Mabele hakuishia hapo kwani aliachia albamu zingine za Soukouss la terreur ya mwaka 1989, Sebene Africa mousso La Femme ivoirienne, Maracas d’or ya mwaka 1988, Réconciliation, Cicatrice na Confirmation.
Japo habari kuhusu familia yake ni finyu sana: Mabele alijaliwa wana ila bintiye kifungua mimba Liza Monet ndiye ajulikanaye sana kwani pia yeye ni mwimbaji wa nyimbo za kufoka foka. Ndio natumai mnaita rap ama hip hop. Yasemekana mkewe Mabele alimwacha baada ya kugundua mumewe alikuwa na ugonjwa wa kiharusi na saratani. Wee!

Miaka ya hivi karibuni Mabele katika umri wa miaka tisini na saba amekuwa akiugua ugonjwa wa saratani ya moyo na tarehe 19 Machi 2020 taarifa kutoka Parii Ufaransa, zilitolewa kwamba Aurlus Mabele amefariki kwa ugonjwa wa COVID-19 unaosabibishwa na Virusi vya Corona ambayo ni janga linaloadhiri mataifa mengi dunia tangu kuanza kwake mwisho wa mwaka 2019 kutoka mji wa Wuhan nchini China.

Ujumbe huu mwanzo ulichapishwa na bintiye Liza Moneta katika mtandao wake wa Twitter na baadaye kudhibitishwa na rafiki zake wa karibu Nyboma Mwandido na Mav Cacharel ingawa meneja wake Jimmy Ouetenoua amesema haijadhibitishwa kwamba aliaga kutokana na virusi hivyo ikizingatiwa alikuwa akiugua magonjwa mengine na bado kuna sitofahamu kuhusu nchi atakapozikwa aidha ufaranza au nchi alimozaliwa Kongo Brazaville. Lakini Corona yaweza kusababisha Aurlus Mabelé kutozikwa Congo.

Ingawa ni makiwa kwa mashabiki wa lingala, kazi, nyimbo na ufanizi wa Aurlus Mabele utakuwa hai na kumbukumbu itakayoelezwa na kuigwa katika vizazi vingi ulimwenguni.

 

aurlus mabélé 2018,

aurlus mabélé songs,

loketo (meaning),

arius mabele,

diblo dibala,

aurlus mabélé mp3 songs,

aurlus mabele songs download,

aurlus mabele songs mp3 free download,

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments